Toka sheria hadi neema by BYUMANINE BISIMWA
Kitabu hiki kinazungumuzia kuhusu sheria na neema, hazina za wema wa Mungu kwa binadamu toka mwenendo wa taifa la Mungu hapa duniani. Sheria ilitolewa na Mungu kwa mkono wa Musa na neema ilitolewa na Mungu kwa mukono wa Kristo.(Yn,1,17). Hizi hazina mbili ni serikali mbili tofauti. Moja ni serikali ya mupito, ndiyo sheria; ingine ni serikali ya milele, ndiyo Neema. Serikali ya mupito ni kama laboratoire (laboratory) ya kuonesha magonjwa pasipo kuponyesha, bali serikali hii ya milele inaonyesha magonjwa na pia ina leta dawa kwa ajili ya uponyaji wa milele, hii ndio "neema".