Uongozi bora by BYUMANINE BISIMWA
Kifupi ya mambo yaliomo katika kitabu hiki ni namuna mbali mbali, tunaokuta katika jamii mbalimbali , ki biblia na kihistoria. Maono yana maana ya kuona mbali, kuepusha kundi na madhara mbali mbali, inayoweza kufikia kundi lenyewe kama halina kiongozi, tena kiongozi mwenye maono. Yesu Kristo kiongozi mwenye maono,ya kufikilia kundi, kuona wapi kundi liko mpaka wapi, na linaelekea wapi. Kwa hiyo ana uchungu kuona kundi linaishi bila mchungaji,kwa kiwango kundi lenyewe linajishugulikia kwa kukosa kiongozi wa kulielekeza. Katka masemi yake , tunakuta akitamka maneno haya ; « mimi ni nuru ya ulimwengu, yeye anayenifuata, hatatembea katika giza , bali atakuwa na nuru ya uzima ndani mwake( Yn 8, 12) Kiongozi mwema anaita kundi limfuate nyuma yake, kwani yeye ndiye anajua wapi atalipeleka kundi lake( Yn 10, 9, 10).